UCHAGUZI MKUU 2020: Ni Zamu Ya Marekani Kuchagua

03Nov 2020
UCHAGUZI MKUU MAREKANI 2020
Nipashe
UCHAGUZI MKUU 2020: Ni Zamu Ya Marekani Kuchagua
  • Nani ataiongoza Marekani kwa miaka minne ijayo? Miji miwili midogo tayari imesha piga kura katika jimbo la New Hampshire

​​​​​​​Huku ni rais aliekuwa madarakani Donald Trump akigombea muhula mwingine wa miaka minne akipepea bendera ya Wanajamhuri (Republicans). Huku ni aliekuwa Makamu wa rais wakati wa uongozi wa rais mstaafu Barack Obama, Joe Biden, akipeperusha bendera ya Wanademokrasia (Democrats)

Nani ataiongoza Marekani kwa miaka minne ijayo? Miji miwili midogo tayari imesha piga kura katika jimbo la New Hampshire.

Ni asubuhi ya Novemba 3 huko nchini Marekani na swali ni moja, Je! Rais aliekua madarakani Donald Trump atashikilia usukani au mgombea urais aliekuwa makamu wa rais Joe Biden atamsukuma nje?

Kinyang’anyiro hiki hakina kukisia, Wamarekani wenyewe wataamua na tayari wameshaanza kupanga mistari nje ya vitu vya kupigia kura .

Bado ni mapema sana kutabiri chochote, kilicho wazi nikwamba huu ni mvutano mkubwa kwani upigaji kura wa leo utaamua hatima ya ya Bunge la Marekani.

 

Wanademokrasia (Demokrats) wanataka kurudi kwenye seneti wakati wa Wajamhuri (Republicans) wanataka kudhibiti nafasi yao.

 

Atakae ibuka kidedea ni nani? Jibu litakuwa wazi baada ya masaa machache tu.

 

Jinsi corona ilivo athiri Uchaguzi 2020

 

Marekani ni kati ya sehemu nyingi duniani ambazo bado zinapambana na janga la Coronavirus. Hali ni mbaya kiasi kwamba kura nyingi zimepigwa kwa njia ya posta.

Watu wengi wameamua kukaa mbali na vituo vya kupigia kura wakihofia msongamano.

 

Hesabu ya kwanza ya kura imeishatoka: Nani anaongoza?

 

Kama jadi, miji miwili midogo kwenye jimbo la New Hampshire zilipiga kura mara tu mkono wa sekunde ulipo pita saa sita usiku.

Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden anaongoza katika mji wa Dixville Notch uliopo kaskazini karibu na mpaka wa Canada, ambapo amepata kura tano.

Upande wapili huko Millsfield, maili 12  Kusini ya Dixville Notch, Rais Donald Trump anaongoza kwa kura 16.

 

Kupata taaarifa zaidi za uchaguzi wa Marekani kadri zinavotoka, bofya hapa: https://epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa