Udasa kuwakutanisha wasomi siku ya uhuru

07Dec 2019
Gwamaka Alipipi
Dar es Salaam
Nipashe
Udasa kuwakutanisha wasomi siku ya uhuru

JUMUIYA ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeandaa mdahalo wa hadhara siku ya jumatatu utakaowaleta wanataaluma na wadau wa maendeleo kujadili na kutafakari nafasi, wajibu, na mchango wa wanataaluma katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Udasa, Dk.George Kahangwa alisema mdahalo huo utaanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mada kuu ni “Miaka 58 ya Uhuru: Wajibu na Mchango wa Wanataaluma Katika Maendeleo ya Taifa”.

Alisema mdahalo huu utatoa nafasi ya pekee na ya kihistoria ya kujadili na kupata mrejesho kutoka kwa watanzania kuhusu mwenendo wa wasomi nchini na matarajio ya watu kwa mtu aliyepata upendeleo wa kuelimika kwa kiwango cha juu.

Habari Kubwa