UDSM yaja na teknolojia mpya za wakulima

09Aug 2020
Happy Severine
SIMIYU
Nipashe
UDSM yaja na teknolojia mpya za wakulima

Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM), kimekuja na teknolojia mpya ambazo zinalenga kuwanufaisha wakulima  na kuwapunguzia adha wanazopata wakati wa uendeshaji  wa shughuli zao.

Dk Athuman Mahinda mhadhili chuo kikuu cha Dar es salaam akionyesha teknolojia waliyoibuni ya kufukuza wanyama waharibifu shambani.

Teknolojia hizo zimeonyeshwa leo katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea kitaifa mkoani Simiyu, ambapo watalamu hao wameonyesha namna ambavyo wamekuja na mbinu mpya ili kuwasaidia wakulima na wavuvi.

Akionyesha mfumo mpya wa manunuzi na uuzaji wa samaki kwa njia ya mtandao, Ester Mhamila Mwanafunzi wa viumbe maji na uvuvi amesema, kwa kutambua adha wanazozipata wavuvi katika kuuza bidhaa zao sokoni wameamua kuwaraisishia huduma.

"Tumeanzisha program ya Fishgenge ambayo wavuvi wataitumia kuuza samaki na wanunuzi kununua samaki kwa bei inayohitajika na kueleweka kupitia 'Application' inayopatika katika simu za mkononi," amesema.

Mhamila amesema kuwa mbali na kufanya manunuzi vile vile mnunuzi atapata nafasi ya kuona aina ya samaki ambao anawahitaji na kujua ana virutubisho vya aina gani ili kumuongezea uelewa mzuri wa virutubishi vilivyopo katika samaki.

Watalamu hao pia wamengeneza teknolojia ya kuzuia wadudu waharibifu katika Maharage ambapo utumia  majani ya mimea badala  kemikali na mazao yanakuwa salama kwa miezi mitatu hadi minne.

"Tunatumia majani ya mimea ya mwarobaini na utupa katika kuhifadhi maharage, majani hayo inatakiwa isagwe vizuri Kisha ikaushwe baadaye mkulima atachanganya na maharage," Joseph Kalonga Mhadhili Msaidizi wa ndaki ya sayansi ya kilimo na uvuvi.

Habari Kubwa