Ufaransa yataka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Mali

04Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ufaransa yataka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Mali

Ufaransa imesitisha operesheni za pamoja za kijeshi na Mali kutokana na mapinduzi ya wiki iliyopita katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Ilisema ushirikiano wowote utasitishwa hadi itakapopata hakikisho kuhusu nchi hiyo kurudisha mamlaka kwa  utawala wa kiraia.

Vikosi vya Ufaransa vimekuwa vikisaidia wanajeshi kutoka Mali, Chad, Mauritania, Niger, na Burkina Faso kupambana na wanamgambo katika eneo la Sahel.

Mnamo Mei 25, mwanajeshi mwenye nguvu za kijeshi wa Mali, Col Assimi Goïta, alimwondoa mamlakani rais wa kiraia wa nchi hiyo

Wiki hii kundi la Afrika Magharibi la Ecowas na Umoja wa Afrika (AU) ziliivua Mali unachama wa Ecowas.

Siku ya Alhamisi wizara ya majeshi ya Ufaransa ilisema kwamba Ecowas na AU wameweka "mfumo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Mali".

 

 

Habari Kubwa