Ufaulu somo la Kiingereza waporomoka

23Nov 2020
Romana Mallya
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Ufaulu somo la Kiingereza waporomoka

WAKATI Herrieth Josephat kutoka Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara akiibuka mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, ufaulu somo la Kingereza umeshuka kwa asilimia 19.39.

Mwaka jana ufaulu wa somo hilo ulikuwa asilimia 76.63 lakini kwa mwaka huu umefikia asimilia 57.24.

Akitangaza matokeo ya mtihani huo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde, alisema wakati ufaulu wa somo hilo ukishuka, ufaulu wa Kiswahili umepanda na kufikia asilimia 87.68.

Msonde alisema takwimu zinaonyesha ufaulu umepanda kati ya asilimia 0.43 hadi asilimia 5.10 katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Maarifa ya Jamii, ikilinganishwa na mwaka jana.

“Somo la Hisabati na Sayansi ufaulu wake umeshuka kidogo kwa asilimia 0.33 na asilimia 0.65 mtawalia ikilinganishwa na mwaka jana,” alisema.

KUMI BORA KITAIFA

Dk. Msonde aliwataja na shule zao kwenye mabano kuwa ni Herrieth Josephat (Graiyaki, Mara), Huma Masala (Kwema Modern, Shinyanga), Gregory Alphonce (Twibhoki, Mara) na Nyambina Musa (Graiyaki, Mara).

Wengine ni Andrew Mabula (Kwema Modern, Shinyanga), Jonas Ayubu (Little Flower, Mara), Emmanuel Marwa (Kwema Modern, Shinyanga), Prosper Tumbo na Yesaya Bendera nafasi ya kumi wote kutoka shule ya God’s Bridge mkoani Mbeya.

WASICHANA 10 BORA KITAIFA

Aliwataja na shule zao kwenye mabano kuwa ni Harieth Josephat (Graiyaki), Fatuma Ismail (Twibhoki, Mara), Nyamwikondo Malisa (Twibhoki, Mara) Mediana Yusuph (Twibhoki, Mara) Assia Iddy (Twibhoki, Mara) na Rahab Marwa (Twibhoki, Mara).

Wengine ni Alamoki Sanga (Rweikiza, Kagera), Maria Edson (Rweikiza, Kagera, Careen Katamuru (Graiyaki, Mara) na Janeth Majula (Samandito, Geita).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA

Dk. Msonde aliwataja wavulana 10 bora kitaifa kuwa ni Huma Masala (Kwema Modern, Shinyanga), Gregory Alphonce (Twibhoki, Mara), Nyambina Suma (Graiyaki, Mara), Andrew Mabula (Kwema Modern, Shinyanga) na Jonas Ayubu (Little Flower (Mara).

Wengine ni Emmanuel Paul (Kwema Modern, Shinyanga), Emanuel Marwa (Kwema Modern, Shinganya), Prosper Tumbo (God’s Bridge, Mbeya), Yesaya Bendera (God’s Bridge, Mbeya) na Mashana Mabao (Twibhoki, Mara).

SHULE 10 BORA KITAIFA

Dk. Msonde alizitaja kuwa ni God’s Bridge (Mbeya), Bunazi Acres (Kagera), Twibhoki (Mara), Kwema Modern (Shinyanga), Graiyaki (Mara), Kemebos (Kagera), Rwekiza (Kagera), St. Anne Maria (Dar es Salaam), Mumtaaz (Mwanza) na Rocken Hill (Shinyanga).

ZILIZOPANDISHA UFAULU

Dk. Msonde ilizitaja shule 10 ambazo zimeongeza ufaulukuwa ni Mwandu Kisesa (Simiyu), Magana (Mara), Ng’hoboko (Simiyu), Tindabuligi (Simiyu), Nonwe (Shinganya), Mwashagata (Simiyu), Idoselo (Simiyu), Giyuki (Simiyu), Ipililo A (Simiyu) na Masanga (Simiyu).

ZILIZOSHUKA UFAULU

Alizataja kuwa ni Chororo (Mtwara), Mpanda (Tanga), Mabawe (Kagera), Mapinduzi (Singida), Ng’wabagalu (Geita), Muhuwesi (Ruvuma), Milidu (Mtwara), Mbwei (Tanga), Udutu (Tabora na Ng’ongolo (Mtwara).

MIKOA ILIYOONGOZA

Dk. Msonde aliitaja kuwa ni Dar es Salaam, Arusha, Simiyu, Katavi, Kilimanjaro, Iringa, Kagera, Morogoro, Pwani na Mwanza.

Mikoa mitatu iliyoongeza ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo, Dk. Msonde aliitaja kuwa ni Simiyu, Mara na Lindi na iliyoshuka mfululizo kwa miaka mitatu ni Mtwara na Singida.

HALMASHAURI 10 ZILIZOONGOZA

Dk. Msonde alizitaja kuwa ni Arusha Jiji, Kinondoni, Mwanza Jiji, Hai, Moshi Manispaa, Ilemela, Bariadi Mji, Arusha, Malinyi na Mlele.

Alisema kwa upande wa halmashauri na manispaa 10 zilizoongoza ufaulu mfululizo kwa miaka mitatu ni Meatu, Butiama, Musoma vijijini, Uvinza, Itilima Vijijini, Kilosa, Chemba, Nachingwea, Bariadi Vijijini na Igunga.

Kwa upande wa halmashauri na manispaa zilizoshuka ufauli mfululizo kwa miaka mitatu, alizitaja kuwa ni Nanyumbu, masasi mji, Iramba, Masasi, Kilindi, Babati vijijini, Mkalama, Newala, Mtwara vijijini, na Temeke.

Habari Kubwa