Uhaba wa mafuta wapaisha bei samaki

13Jan 2021
Christina Mwakangale
Dar es Salaam
Nipashe
Uhaba wa mafuta wapaisha bei samaki

KUPANDA kwa bei ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini kumesababisha kitoweo cha samaki kuuzwa kati ya Sh. 1,500 hadi 2,000 kwa fungu moja kutoka Sh. 1,000 hapo awali, katika Jiji la Dar es Salaam.

Nipashe ilitembelea maeneo tofauti ya jiji hilo, ambako huuzwa samaki waliokaangwa na kuuzwa kwa mafungu, ikiwamo Soko Kuu la Samaki la Kimataifa la Feri, Buguruni, Gongo la Mboto, Tegeta, na kukuta bei imepanda tofauti na wiki chache zilizopita.

Wakizungumza na Nipashe, mmoja wa wauzaji wa samaki hao, Musa Halfan, ambaye ni mkazi wa Mombasa alisema jana alinunua mafuta pamoja na samaki kwa bei ya juu, tofauti na wiki moja iliyopita.

Halfani alisema: “Jana nimekutana na kitu ambacho sikukitarajia, nimekuta samaki wanauza bei ya juu na mafuta pia. Imenibidi nami nipandishe bei, fungu moja la samaki waliokaangwa nauza kati ya Sh. 1,500 hadi 2,000 kulingana na aina,” alisema Halfan.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa