Ujangili ulivyoua faru kutoka 10,000 hadi 15

27Dec 2020
Sanula Athanas
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Ujangili ulivyoua faru kutoka 10,000 hadi 15
  • *Harakati sasa zalenga wafike 200 *Silaha za kivita, majangili wanaswa *Leo mwaka kifo cha 'bibi' Faru Fausta

KATIKA tafsiri ya nguzo kuu za uchumi wa Tanzania, utalii una nafasi kubwa. Takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonesha sekta hiyo sasa inachangia robo ya fedha za kigeni na asilimia 17.5 ya Pato la Taifa.

Kadri mtu anavyozama kuuchambua utalii huo, anakutana na makundi makuu ya wanyamapori ambao ndiyo vivutio vinavyosafirisha wageni kutoka mbali kuja kuwashuhudia.

Katika makundi hayo, kuna wanyama wakubwa watano ambao ni tembo, faru, twiga, nyati na simba.

Unapomtaja mnyama faru, hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kwanini? Wanyama hao  ambao wamekuwa kivutio kikuu cha watalii, wamekuwa katika hatari ya kutoweka kiasi cha kutikisa mwelekeo wa taifa.

Wakati kuna mtazamo wa jumla, katika mustakabali wa kipekee, leo ni siku maalum kwa wadau wote wa wanyamapori na washirika wa sekta ya utalii, kwa maana ya kumbukumbu ya mwaka mmoja kamili tangu kifo cha Faru Fausta.

Huyu ni aliyekuwa faru mzee zaidi si tu kwa Tanzania, bali kwa dunia nzima akishikilia rekodi hiyo. 

Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Philbert Ngoti, anasema udhalimu umewakumba wanyamapori hao hata wakapungua kutoka 10,000 waliokuwapo nchini miaka ya 1970, ndani ya miaka 30 wakabaki 15 tu.

Pia, takwimu za Shirika la Uhifadhi Duniani (IUCN), zinabainisha kuwa katika miaka ya 1970 Tanzania ilikadiriwa kuwa na faru 10,000 huku Hifadhi ya Taifa Serengeti pekee ikiwa na wanyama hao wapatao 700. Tayari shirika hilo limeshatangaza kuwa wanyama aina ya faru weusi ambao wako 750 katika Ukanda wa Afrika Mashariki, ni miongoni mwa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani.

Vilevile, Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF), linabainisha kuwa Tanzania imepoteza takribani asilimia 99 ya faru weusi katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Sababu ni nini? Ngoti ambaye ni Mratibu wa Faru nchini, anawanyooshea kidole majangili kuwa ni sehemu ya mzizi wa tatizo lililobadili historia ya nchi na hata kuelekea kuwa hasi zaidi...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa