Ukatili kwa watoto washamiri Longido, atua za chukuliwa

29May 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
Ukatili kwa watoto washamiri Longido, atua za chukuliwa

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha Bi. Atunagile Chisunga, amesema kuwa matukio ya ukatili kwa watoto wilayani hapa yanaendelea kukua kwa kasi huku watoto wengi wakikosa sehemu ya kuelekeza malalamiko yao.

Amesema baada ya kubaini hilo, ameamua kuweka utaratibu wa kutembelea katika Shule za Msingi ndani ya wilaya hiyo na kuzungumza na wanafunzi namna ya kuripoti matukio ya kikatili wanayofanyiwa na wazazi, ndugu au walezi wao.

Kauli ameitoa leo Mei 29,2019 alipotembelea Shule ya Msingi Eworendeke na kufanikiwa kubaini uwepo wa mtoto mmoja aliyefanyiwa matukio ya kikatili na mama yake wa kambo.

Mtoto huyomwenye umri wa miaka saba (jina limehifadhiwa) ni mwanafunzi wa awali katika shule hiyo.

Baada ya kubaini jambo hilo, Bi. Atunagile ameshirikiana na Jeshi la Polisi Kata ya Namanga kwa kuhakikisha mtuhumiwa huyo anapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa mahojiano zaidi. 

Ameeleza kuwa wamempeleka mtoto huyo Hospital ya Kata ya Namanga kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo mama huyo aliyefahamika kwa jina la Doreen Mvungi mkazi wa makao mapya Kata ya Eworende mwenye umri wa miaka 19 kabila mpare kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi kituo cha Namanga

Kwa mujibu wa mtoto anadai kuwa ni tabia ya mama huyo wa kambo kumpiga mara kwa mara pasipo sababu yoyote ile na wakati mwingine kumnyima hata chakula.

Habari Kubwa