Ukeketaji chanzo cha utapiamlo Longido

13Aug 2019
Zanura Mollel
ARUSHA
Nipashe
Ukeketaji chanzo cha utapiamlo Longido

Imeelezwa Ukeketaji kwa wanawake wilayani Longido mkoani Arusha imekuwa chanzo cha ukosefu wa lishe bora kwa kinamama wajawazito kutoka jamii ya kifugaji (Maasai) kutokana na mila na desturi ya jamii hiyo inayowataka kutokula vyakula vyenye virutibisho ili wakati wa kujifungua wasipate matatizo.

Afisa kutoka Shirika la Tembo Trust Mary Laizer.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa kutoka Shirika la Tembo Trust Mary Laizer katika semina ya kamati ya lishe wilayani humo na kusema sababu ya jamii kuwanyima wajawazito lishe bora ni kuwawezesha kujifungua watoto wadogo.

"Vifo vinaongezeka kutokana na hali ya ukeketaji kwani madhara ni makubwa vifo vya mama na mtoto wakati na hata baada ya kujifungua kutokana na kumwaga damu nyingi, afya duni kwa kukosa lishe bora" amesema Laizer

Awali Afisa Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Maria Ngilisho amesema tafiti zimeonyesha watoto na watu wazima waliowahi kukabiliwa na tatizo la Utapiamlo kuwa ubongo wao wa kufikiri ni mdogo sana (ubongo mdogo) tofauti na ambao hawajawahi kabiliwa na tatizo hilo.

Habari Kubwa