Ukosefu elimu,mfumo dume chanzo kukandamiza wanawake vijijini

17Oct 2021
Yasmine Protace
Nipashe Jumapili
Ukosefu elimu,mfumo dume chanzo kukandamiza wanawake vijijini

IMEELEZWA kuwa ukosefu wa elimu ikiwamo na kuwapo kwa mfumo ndume,kumchangia kuwadidimiza wanawake wa vijijini katika kufanya maamuzi ikiwamo kumiliki ardhi.

Hayo yamesemwa na Hasan Juma ambaye ni mmoja wa washiriki wa demina za Maendeleo ya Jamii( GDSS) ambazo ufanyika kila jumatano Jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na TGNP Mtandao.

Juma ambaye alishiriki katika mada iliyotolewa na Rehema Mwateba,ambapo mada ilihusu siku ya wanawake vijijini nini maoni ya waoni ya wana GDSD kuhusu siku hiyo.Juma anasema mwanamke wa kijijini amesaulika sana tofauti na mwanamke wa mjini.

" Mwanamke wa kijijini  mzalishaji mkubwa wa chakula,lakini maisha anayoishi sio sawa na mwanamke wa mjini," anasema. Suleimani Bishagazi anasema  elimu itolewe kwa wanawake wa vijiji  ili waweze kuzijua haki zao.

Anasema mwanamke wa Kijiji pamoja na kuwa mzalishaji chakula lakini bado anakabiliwa na changamoto ya kumiliki ardhi.

Mwanamke wa kijijini anakabiliwa na changamoto katika masuala ya miundombinu,afya ikiwamo na elimu.

Rehema Mwinyi anasema kuwa mwanamke wa kijijini amesaulika hata katika maamuzi hashirikishwi.

Anaongeza kuwa mwanamke wa kijijini pamoja na kuwapo na changamoto  zinazokabili jamii yote iwe ya mjini au kijijini,lakini kwa mwanamke wa kijijinihuwa anakabiliwa na changamoto kubwa.

Anasema wanawake wanatoa mchango mkubwa katika kutunza familia ikiwamo na uzalishaji wa kilimo.

Anasema idadi kubwa ya umasikini vijijini niya juu zaidi ikilinganishwa na mjini,licha ya kuwa wanazalisha kilimo.

Anasema katika sekta ya kilimo wanawake wa vijijini uzalisha ,lakini uwezo wa kuomba Mikopo katika mabenki hawana hata baadhi yao uuza bidhaa za na pesa wakipata uziweka katika kibubu ambapo usalama wake unakuwa ni mdogo.

Anaongeza kuwa katika suala la ajira vijijini kunakuwa na pengo kubwa ambapo wanawake katika ajira wanakuwa wachache kuliko wanaume.

Anasema wanawake wengi wa vijiji I wanaishi bira ya kuwa na usalama ikiwamo kukabiliwa na ubaguzi  pamoja na vurugu na migogo ya kiuchumi ,shida ya chakula na MABADILIKo ya Tania nchi.

Anasema wengi wao wanawake wa vijijini wanakabiliwa na  changamoto za miundombinu ,huduma za afya,elimu na kutoshirikishwa katika maamuzi.

Rehema  Mwateba ambaye alikuwa mtoa mada kwa washiriki wa GDSS anasema kuwa  wanawake wa vijijini wanatakiwa kukuzwa kiuwezo ikiwamo na kijamii.

Anasema mwanamke hatakiwi kuwa na shida yoyote  katika masuala ya kijamii ,elimu,maji na kiutamaduni..

Anadema mwanamke anatakiwa kukuzwa kiuchumi, ili kuwepo na ushiriki wa wanawake katika mikutano yao  na wanapotoa maoni yao wayachukuwe na kuyafanyia kazi.

Habari Kubwa