Ukosefu wa vifungashio changamoto kwa wajasiriamali

16May 2019
George Tarimo
IRINGA
Nipashe
Ukosefu wa vifungashio changamoto kwa wajasiriamali

IMEELEZWA kukosekana kwa vifungashio ni chanzo cha kuathiri soko la bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo mkoani Iringa kutokana na kutumia vifungashio visivyokidhi vigezo na ushindani katika soko.

Wakizungumza na Nipashe mara baada ya kukamilika kwa kongamano la wajasiriamali na wanunuzi wamesema pamoja na kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi viwango bado ukosefu  wa vifungashio unachangia  bidhaa hizo kukosa ushindani wa masoko na  mvuto kwa walaji wan je ya mkoa .

Wakizungumza wajasiriamali Theodori Msigala na Genoveva Barnabas wameomba wajasiriamali kuungana kwa lengo la kuagiza vifungashio nje ili kupunguza gharama.

Msigala alisema wapo baadhi ya wafanyabishara wakubwa wanauliza kwanini hawaoni bidhaa kutoka Iringa? Lakini jibu la haraka bidhaa za Iringa zipo sokoni lakini changamoto kubwa ni kukosekana na vifungashio na kutangazwa ipasavyo.

Stela Mdahila ni meneja wa mradi wa Tanzania Local Enterprise Development  (TLED) amesema  mkoa wa Iringa una zaidi ya  wajasiriamali 460 lakini changamoto kwa wajasiriamali hao ni ugumu wa upatikanaji wa masoko ya uhakika wa bidhaa wanazozalisha.

Alisema kuwa lengo kuwa la mradi ni kuhakikisha wanunuzi,wauzaji wanakaa pamoja mezani,wanajadili kwa pamoja na baadaye wanatoka na maazimio juu ya kupata vifungashio,masoko ya uhakika ndani nan je ya mkoa ikiwezekana hata nje ya nchi.

Habari Kubwa