Ulega atoa milioni 10 kusaidia kampeni serikali za mitaa

11Nov 2019
Dotto Lameck
Pwani
Nipashe
Ulega atoa milioni 10 kusaidia kampeni serikali za mitaa

MBUNGE wa Mkuranga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Ulega, ametoa shilingi milioni 10 na vifaa kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo lake unaotarajika kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

Ulega ametoa fedha na vifaa hivyo vikiwemo spika 25, bendera 1,380 za chama, kadi 3,000 za uwanachama, jezi na mipira 18 katika mkutano mkuu maalumu wa CCM Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani uliohudhuriwa na Katibu wa Nec, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanal Mstaafu Ngemela Lubinga. 

“Nakabidhi fedha taslimu shilingi milioni 10 na vifaa hivi kwa ajili ya kustawisha chama kwa matawi 247 katika jimbo langu hasa kwa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa” amesema Ulega.

Naye Katibu wa Nec, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanal Mstaafu, Ngemela Lubunga, amewasihi wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi katika uchanguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa ni haki yao ya msingi.

Habari Kubwa