Ulinzi waimarishwa ujio wa viongozi EAC

01Mar 2016
John Ngunge
ARUSHA
Nipashe
Ulinzi waimarishwa ujio wa viongozi EAC

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amesema
wameimarisha ulinzi mkoani hapa ili kufanikisha ujio salama wa
viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
wanaotarajiwa kuwasili mkoani hapa leo.

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas

Wakuu hao wanatarajia kuanza kikao cha kawaida cha Jumuiya hiyo katika
mkutano wa 17 kesho.

Akizungumzia hali ya ulinzi, Kamanda Sabas alisema: “Tumejipanga
wageni wawasili salama, wafanye mkutano salama kisha warejee salama
makwao.”

Aliwaomba wananchi kushirikiana na polisi kufichua uhalifu na
wahalifu katika kipindi chote ambacho viongozi hao watakuwapo mkoani
hapa. Alisema ulinzi utakaotumika ni pamoja na wa mbwa.

Msemaji wa EAC, Othieno Richard Owora, alithibitisha kuwa viongozi wa jumuiya hiyo watahudhuria mkutano huo.

Habari Kubwa