Ummy atoa miezi mitatu matumizi mifuko ya plastiki

23Feb 2021
Dotto Lameck
Tanga
Nipashe
Ummy atoa miezi mitatu matumizi mifuko ya plastiki

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu, ametoa agizo kwa watu ambao watabainika kutumia vifungashio vya mifuko ya plastiki baada ya miezi mitatu aliyoitoa kupita wakamatwe na kuchukuliwa hatua.  

Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa katika ziara yake jijini Tanga iliyotokana na malalamiko yaliyopo katika Jiji hilo kuhusiana na uchafuzi wa mazingira unaotoka katika viwanda vya kuzalishia saruji na chokaa.Ummy amesema kuwa suala hilo la vifungashio alikwisha kutoa miezi mitatu litakuwa limekwisha ambapo ni hadi kufikia April Mwaka huu hategemei kuona matumizi ya vifungashio vya plastiki yakiendelea.

“Nisisitize suala la vifungashio nilitoa miezi mitatu hivyo mwezi wanne litakuwa limekwisha baada ya miezi mitatu kuisha tutatoa agizo la kuwaambia mkamatwe kwa yeyote ambaye anatumia vifungashio maana mifuko ya plastiki imerudi kwa kigezo cha vifungashio.”amesema Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amezitaka Halmashauri zote ziandae mpango kazi wa Mazingira ambao utakuwa na tija kubwa katika kusimamia na utekelezaji wa kazi hizo kwenye maeneo yao.

Habari Kubwa