Upanuzi Bandari Dar waanza

06Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Upanuzi Bandari Dar waanza

Kazi ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam imeanza, ambapo kukamilika kwake itaweza kuhudumia meli zenye urefu wa zaidi ya mita 250 na kina cha mita 14.5 ifikapo mwaka 2020.

Taarifa kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), inasema kwa sasa kazi ya upimaji uimala wa udongo unaendelea kabla ya kujenga nguzo kwa ajili ya gati la kuhudumia magari.

Kukamilika kwa ujenzi wa gati hiyo kutaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam wa kuhudumia shehena kutoka tani milioni 15 za sasa hadi tani milioni 28 kwa mwaka.

Kadhalika, Bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba makasha 8,000 kutoka 2,500 ya sasa ifikapo mwaka 2028.

Habari Kubwa