Upelelezi kesi ya mauaji mwanaharakati tembo bado 

14Feb 2018
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Upelelezi kesi ya mauaji mwanaharakati tembo bado 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam juzi iliambiwa upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo na Mkurugenzi wa PALMS Foundation, Wayne Lotter, inayowakabili watu watatu akiwamo Meneja wa Benki, Khalid Mwinyi, bado haujakamilika.

Wayne Lotter.

Mbali na Mwinyi, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Rahma Almas (Baby) na mchimba makaburi Mohammed Maganga.

Kesi hiyo ilipangwa kutajwa juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbard Mashauri.

Wakili wa Serikali, Saada Mohamed, alidai kuwa kesi ilipangwa kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika. 

Hata hivyo, mshtakiwa  Almas alidai kuwa mshtakiwa Maganga ni mgonjwa ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mashauri alisema  kesi hiyo itatajwa Februari 21,mwaka huu, na washtakiwa wataendelea kukaa rumande.Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya makusudi.

Ilidaiwa kuwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie, Kinondoni jijini Dar es Salaam, walimuua kwa makusudi Wayne Lotter. 

Habari Kubwa