Upimaji sampuli corona sasa maabara mpya Mabibo

23May 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR
Nipashe
Upimaji sampuli corona sasa maabara mpya Mabibo

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kueleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na Kamati teule ya Uchunguzi.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Amebainisha kuwa kamati imegundua uwepo wa mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19.Amesema "Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati"Amesema "Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii"

"Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1,800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu"Aidha, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo, DSM na kuzungumza na madereva wa malori na kuwahakikishia kupata majibu ya Covid-19 ndani ya masaa 24 

Habari Kubwa