Usalama mdogo wa chakula chanzo cha magonjwa yasiyoabukizwa

21Nov 2021
Neema Emmanuel
Mwanza
Nipashe Jumapili
Usalama mdogo wa chakula chanzo cha magonjwa yasiyoabukizwa

​​​​​​​USALAMA mdogo wa chakula chanzo cha magonjwa yasiyoabukizwa nchini huku kundi la vijana likitajwa kuongoza kwa vifo na ulemavu wa kudumu.

Kwa mujibu wa Takwimu za Kamishna ya umaskini na magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (NCDIs) zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la asilimia 41 ya vifo na majeruhi nchini hali inayochangia upotevu wa nguvu kazi.

"Magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, saratani mbalimbali pamoja na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa ndio imechangia ongezeko hilo kuwa mara mbili ya hali iliyokuwepo miaka 25 uliyopita huku theluthi mbili ya tatizo hili likiwa kwa watu walio chini ya miaka 40 " takwimu zinaeleza.

Pia imeeleza kuwa mtazamo tofauti uliopo kuwa kundi la wazee ndio linaloongoza kwa kuugua magonjwa hayo ni tofauti kwa sasa baada ya takwimu kuonyesha ongezeko kubwa la magonjwa hasa ya shinikizo la damu na kiharusi likiwapata vijana.

Imeelezwa kuwa mikakati iliyopo ya kwa sasa ya kupambana na tatizo hilo ni inazingatia tiba kuliko kinga hiyo ni baada ya wananchi kuweka mkazo kwenye kutibu zaidi kuliko kukinga.

"Ugonjwa huu sio wa matajiri na wazee kwa mujibu wa tafiti kwa sasa yanaathiri na watu maskini wanaoishi vijijini hapa nchini, sasa wakati umefika wa wananchi kutambua visababishi vya magonjwa haya ni tabia za aina nne ambazo ni matumizi ya tumbaku,kutofanya mazoezi,ulaji vyakula usiozingatia lishe bora na matumizi ya pombe kupita kiasi visababishi hivi huchangia asilimia 80 ya tatizo hili duniani" Tafiti zinaeleza.

Pia sekta ya afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watashirikiana kuchukua hatua madhubuti na zinazohusisha sekta mbalimbali ili kupambana na tatizo hilo ,kuokoa maisha ya wananchi ili kuwa na taifa lenye afya litakalokuwa chachu katika kukuza uchumi binafsi na wataifa .

Habari Kubwa