Ushauri wa Profesa Assad kwa CAG Kichere

05Nov 2019
Beatrice Shayo
Dar es Salaam
Nipashe
Ushauri wa Profesa Assad kwa CAG Kichere

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mussa Assad, amekabidhi ofisi kwa CAG mpya Charles Kichere na kumshauri asikimbilie kufanya mabadiliko itaathiri Taasisi hiyo muhimu.

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mussa Assad.

Kadhalika, Prof. Assad amesema kwa sasa anahamia shambani kwake kwa ajili ya shughuli za kilimo atakapohitajika mjini atakuja.

Prof. Assad ameyasema hayo leo wakati akikabidhi ofisi kwa CAG Kichere jijini Dar es Salaam.

"Naamini sikufanya mabadiliko mimi huwa naamini changes huwa zinaweza kutokea lakini zitokee katika namna ambayo zimepangwa vizuri sikuwa mwaminifu wa ule mfumo wa kutoa watu wote na kuweka wengine," alisema Prof. Assad.

Prof. Assad alisema kufanya mabadiliko inahitaji gharama kubwa, hivyo Kichere ukifanya mabadiliko kwa haraka utapoteza historia ya Taasisi hiyo.

Habari Kubwa