Utafiti: Wengi hawajui kama wanaumwa meno

21Nov 2020
Neema Emmanuel
Mwanza
Nipashe
Utafiti: Wengi hawajui kama wanaumwa meno

UTAFITI wa kitalaam unaonyesha kwamba wananchi wengi  wana matatizo ya kinywa na meno licha ya kuwa wenyewe hawajui.

Hayo yamebainishwa juzi na daktari bingwa wa upasuaji wa shingo, kichwa na  meno kutoka Hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando, Dk. Emmanuel Motega.

Dk. Motega alisema utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi wana matatizo ya kinywa na meno na kwamba  wanaishi na matatizo hayo.

Sababu kubwa, kwa mujibu wa daktari bungwa huyo, ni kuwapo kwa uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo huku akiwaomba wananchi wanapohisi maumivu  ya  meno, harufu mbaya ya kinywa, kuwahi hospitalini.

Alisema mtu akichelewa kupata matibabu,  bakteria huingia sehemu zingine za mwili na kusababisha magonjwa mengine kama moyo, majipu ya kashuka kwenye shingo au kifuani, uvimbe na saratani.

"Kwa sasa huduma ya meno imeboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu kwani tunaweza kutibu jino bila kung'oa. Tunaweza kuziba meno, kusafisha fizi ambazo zimepata magonjwa, kufanya upasuaji wa shingo na kichwa," alisema Dk. Motega.

Habari Kubwa