Utekelezaji mradi bomba la mafuta kuanza Aprili

12Apr 2021
Dotto Lameck
Dodoma
Nipashe
Utekelezaji mradi bomba la mafuta kuanza Aprili

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amesema utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga-Tanzania hadi Uganda utaanza mwezi huu wa Aprili na sio Julai kama ilivyokuwa imepangwa awali.

WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani.

Dk. Kalemani amesema hayo leo April 12, 2021 Bungeni jijini Dodoma, baada ya Mbunge wa Kiteto, Edward Lekaita kuuliza swali la nyongeza."Tunaanza rasmi ujenzi mwezi huu na kwa muda wa miaka mitatu. Nilishiriki utiaji saini utekelezaji wa mradi huu na Rais Samia Suluhu Jana Nchini Uganda" amesema Dk. Kalemani.Aidha, amesema mradi huo utapita katika Mikoa nane, Wilaya 24, Vijiji 127 na Vitongoji 502. Kwa mujibu wa Dk. Kalemani, mradi utatoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 10,000 katika hatua za awali na hadi ajiri za Watanzania 15,000 katika shunguli za ujenzi.

Pia, Dk. Kalemani amewaomba Wananchi ambao wapo karibu na mradi huo kujitokeza kuchukua fursa hizo kwa sababu zimewekwa rasmi kwa ajili ya Watanzania.

Habari Kubwa