UVCCM Hai watuma salamu kwa Mbowe

25Jun 2019
Na Mwandishi Wetu
HAI
Nipashe
UVCCM Hai watuma salamu kwa Mbowe

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, Cedrick Pangani amesema vyama vya upinzani visipoteze muda kufanya kampeni katika jimbo hilo katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwani jimbo hilo litakuwa chini ya chama tawala.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akimsikiliza Mwenyekiti wa UVCCM wiaya hiyo Cedrick Pangani alipomtembelea ofisini kwake.

Amezungumza hayo leo na The Guardian Digital baada ya kukutana na Mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya ofisini kwake. Pangani amesema wananchi wa Hai wasimuangushe Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwani hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi pamoja na wa mtu mmoja mmoja hivi sasa.

"Leo nimemtembelea kiongozi wetu ( Lengai Ole Sabaya ) baada ya maneno mengi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha taarifa ambazo sio za kweli kuwa amepata ajali mimi niwahakikishie wana CCM kuwa kiongozi wetu yupo salama sisi tuchape kazi kwani yeye ana imani kubwa na na sisi katika kuifanya Hai kuwa chini ya CCM kwani muda wa upinzani umekwisha," Amesema Pangani

Amesema kuwa ni ukweli usiopingika na hata wapinzani wanafahamu hilo kuwa kwa miaka mitano ya uongozi wa Rais John Magufuli nchini imepata heshima kubwa Afrika na Duniani kwa maendeleo makubwa ya haraka hasa katika kukuza uchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii katika maeneo mengi nchini. 

"Hai tunakuja na kauli mbiu yetu ya HAI YA KIJANI huu ni mkakati wetu kuhakikisha CCM tunaendela kuwaletea maendeleo wana Hai, mimi niwasihi wananchi wa jimbo letu wala msipoteze muda kusikiliza sera za upinzani kwani hazieleweki wao wamekalia kulalamika tu ni wazi hakuna kitu walichofanya kwa kipindi chote.Sasa ni wakati wetu kuwahudumia wananchi ni sasa," Amesema Pangani na kuongeza kuwa;  

"UVCCM wilaya ya Hai, tunamshukuru sana kiongozi wetu komredi Sabaya kwa jinsi anavyoshirikiana na sisi katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo wilayani hapa pia tuna muhakikishia kuwa tupo timamu kuhakikisha tunalinda heshima ya Rais Magufuli, heshimma yake pamoja na chama," Amesema 

Habari Kubwa