UWT Longido wamshukuru Rais Magufuli

18Jun 2019
Zanura Mollel
Longido
Nipashe
UWT Longido wamshukuru Rais Magufuli
  • Ni kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali ya wilaya
  • Hospitali hiyo inatarajiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Longido mkoani Arusha imemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa fedha Shilingi Billion 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya hiyo inayotarajiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Wajumbe Wa kamati ya siasa UWT Wilaya walipoitembelea hospital ya Wilaya hii Leo kwa lengo la kukagua shughuli za ujenzi.

Akizungumza na Nipashe hii leo baada ya kikao cha kamati ya siasa ya UWT ,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sinyati Ngobey alisema kuwa kuwepo kwa hospital ya wilaya kutapunguza vifo vya mama na mtoto kwani huduma zote za afya zitapatikana. 

Alidai kuwa hospital ya kata ya Longido ambayo kwa sasa inatumika kama hospital ya wilaya haina vifaa vyote vya matibabu hivyo wagonjwa wengi hulazimika kupelekwa hospital ya rufaa  Mount Meru mkoani Arusha kwa matibabu zaidi.

" Mama mjamzito hadi afikishwe hospital ya Mount Meru kwa huduma zaidi anaweza kupoteza maisha ,kwani kutokea hapa Longido hadi Arusha ni km 80 kuna umbali sana,kwa kweli tunamshukuru sana Mh Rais " alieleza Sinyati

Naye Katibu wa UWT wilayani Longido Judith Laizer alisema kuwa serikali imejenga majengo saba hadi sasa kwenye hospital hiyo, kwa kutumia Billion 1.5 lakini kupitia ziara ya ghafla aliyoifanya Waziri Wa TAMISEMI Seleman Jaffo wilayani hapa alisema kuwa ataiongezea hospital hiyo sh Million mia 5 kwa ajili ya kumalizia hospital hiyo.

Katibu Wa UWT Wilaya  Longido akikagua ujenzi unaoendelea wa hospital ya Wilaya.

" Serikali imetuongezea pia million mia tano kwa ajili ya kumalizia ujenzi na hii ni kutokana na usimamizi mzuri Wa viongozi Wa Wilaya chino ya Dc Mwaisumbe"

Alidai kuwa majengo yaliyo jengwa ni jengo la mama na mtoto,jengo la wagonjwa Wa nje,wodi ,jengo la upasuaji ,jengo la utawala na kuwataka wananwake Wilayani hapa kuacha Tabia ya kujifungulia majumbani .

Mwenyekiti wa UWT Wilaya Sinyati Ngobey akikagua ujenzi wa hospital ya Wilaya.

"Niwaombe wanawake wakati hospital hii inaendelea kukamilika katika hatua ya ujenzi tumieni vituo vya afya vilivyopo ndani na nje ya Wilaya kwa ajili ya matibabu, ili kupunguza kasi ya vifo vya mama na mtoto" aliomba Judith

Habari Kubwa