Vifo majeruhi ajali ya lori la mafuta vyafikia 101

23Aug 2019
Mary Geofrey
Dar es Salaam
Nipashe
Vifo majeruhi ajali ya lori la mafuta vyafikia 101

IDADI ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya moto wa lori la mafuta iliyotokea Morogoro, imeongezeka na kufika 101 baada ya majeruhi mwingine mmoja kufariki dunia leo alfajiri wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH Aminiel Aligaesha.

Kufuatia vifo hivyo, idadi ya majeruhi waliosalia Muhimbili ni 14 kati ya majeruhi 47 waliopokelewa hospitalini hapo Agosti 10 mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH Aminiel Aligaesha, akizungumza na waandishi wa habari leo amesema kati ya majeruhi hao 11 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wakiendelea kupatiwa matibabu na wengine watatu wapo wodi za kawaida.

Amesema majeruhi watatu wameanza kufanya mazoezi ya viongo kutokana na hali yao kuimarika

Amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Sadick Buganga (32).

 

Habari Kubwa