Vijana Katavi wapewa elimu ujasiriamali, afya ya uzazi

09Jul 2020
Neema Hussein
KATAVI
Nipashe
Vijana Katavi wapewa elimu ujasiriamali, afya ya uzazi

Vijana zaidi ya 1,000, katika Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, wamepewa elimu ya ujasiliamali na afya ya uzazi lengo ikiwa nikupunguza au kuondoa kabisa mimba za utoto na vijana kutojishughulisha.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, Seleman Mtenjela Ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo.

Akizungumza katika mafunzo yaliyowashirikisha waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Hope Center Tanzania linalo jihusisha na utoaji wa elimu  kwa vijana, Halima Lila, amesema vijana wengi wa Katavi hawana elimu hiyo jambo ambalo linapelekea kushindwa kutimiza ndoto zao.

Amesema kutokana na mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya matukio ya mimba za utotoni na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa ni sababu ambayo wao kama shirika imewafanya waone umuhimu wa kuwafanya vijana wajitambue.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Hope Center Tanzania linalotoa elimu ya Ujasiliamali na Afya ya Uzazi kwa vijana, Halima Lila akizungumza na wandishi wa habari kushirikiana kutokomeza mimba za utotoni ni kufanya vijana wajitambue

Lila amesema vijana wengi hawajui kama kuna mikopo katika Halmashauri zao ambayo inahusu vijana kupitia shirika hilo ambalo liliwapa elimu vijana juu ya kutumia mikopo hiyo inayotolewa na serikali. 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Seleman Mtenjela, ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo akimuwakilisha Mkurugenzi wa Tanganyika, amesema wilaya hiyo ina idadi kubwa ya vijana waliopata magonjwa ya dhinaa kama vile Kaswende, Gonolea na HIV.

Amesema hawataweza kufikia malengo kama kutakuwa na vijana ambao hawajitambui,hawajui kutumia fursa zilizombele yao wala kutokujua  afya ya uzazi haswa kwenye swala ya uzazi wa mpango.

 

Habari Kubwa