Vijiji vyote kung’ara umeme 

07Dec 2017
Yasmine Protace
Nipashe
Vijiji vyote kung’ara umeme 

SERIKALI imetenga zaidi ya Sh. bilioni 30 kwa ajili ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia mradi wa REA awamu ya tatu katika mkoa wa Pwani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgallu, alisema hayo alipokuwa akizindua mradi wa umeme jua kisiwani Kwale Kisiju, wilayani Mkuranga.

“Katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unakua siku hadi siku, serikali  imetenga zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa mkoa wa Pwani, kwa ajili ya kuhakikisha unapatikana umeme wa REA awamu ya tatu,” alisema.

Aliongeza kupatikana kwa umeme huo kutasaidia shughuli za uchumi hususan viwanda.

Alisema watu wa pembezoni mwa bahari wana mahitaji makubwa ya umeme, hivyo watahakikisha nishati hiyo inapatikana ili kuboresha maisha yao.

Mgallu alizitaka taasisi zichangamkie fursa kutokana na serikali kupeleka maendeleo katika vijiji ili kubadilisha maisha.

Katibu Mkuu wa asasi ya Tandem Trust, Cheistian Shembilu, ambayo imepeleka mradi huo, alisema mradi umetumia zaidi ya Sh. milioni 200 na kuwa kazi yao ni kuhamasisha maendeleo ya jamii. 

Habari Kubwa