Vilio vyatawala mapokezi madereva waliotekwa Congo

22Sep 2016
Beatrice Shayo
Nipashe
Vilio vyatawala mapokezi madereva waliotekwa Congo

MADEREVA wawili, Selemani Fumbuka na Hamis Mshana waliofanikiwa kulitoroka kundi la waasi wa Mai Mai la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wameeleza jinsi walivyofanikiwa kujinasua dhidi ya kundi hilo.

Madereva wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao, baada ya kuwasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana baada ya kuokolewa kutoka kwa kikosi cha waasi cha Mai mai nchini Kongo. PICHA: HALIMA KAMBI

Fumbuka na Mshana ni miongoni mwa madereva 15 (10 wa Tanzania na watano wa Kenya) waliotekwa Septemba 14 na kundi hilo lililochoma magari yao na kutaka lipewe dola za Marekani 5,000 kwa kila mmoja ili liwaachie, vinginevyo lingewaua kama kiasi hicho cha fedha kisingetolewa ndani ya saa 24.

Mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana saa 9:50 alasiri, vilio vya furaha vilitawala kwa ndugu wa madereva hao.

Kwa maelezo zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO

www.guardian.co.tz/circulation

Habari Kubwa