Viongozi dini, serikali waonya maandamano

01Nov 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Viongozi dini, serikali waonya maandamano

MCHUNGAJI wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini, John Kilinda, amewataka wagombea ambao wameshindwa kwenye uchaguzi mkuu na hawakurudhika na matokeo, wapinge kisheria badala ya kuandamana.

Wakati kiongozi huyo wa dini akitoa kauli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, amevitaka vyombo vya doka kuwadhibiti wanasiasa na wafuasi wanaochochea vurugu na maandamano kwa madai ya kutoridhuika na matokeo ya uchaguzi.

Kilinda alisema hayo jana wakati wa ibada ya jana kanisani hapo kuwa wanamshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao na hatimaye uchaguzi umemalizika kwa amani.

Alisema uchaguzi umeshamalizika na washindi wamepatikana, hivyo wakiwa viongozi wa dini, hawataki kusikia kuwapo kwa viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani, kutoka kwa wagombea ambao wameshindwa.

"Uchaguzi mkuu umemalizika kwa amani, hivyo nitoe rai kwa wagombea ambao wameshindwa na hawakuridhika na matokeo, wasiingie barabarani bali wapinge matokeo hayo kisheria," alisema Mchungaji Kilinda ............kwa habari zaidi fuatilia epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa