Viongozi saba wa upinzani mbaroni kwa tuhuma za ugaidi

02Nov 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Viongozi saba wa upinzani mbaroni kwa tuhuma za ugaidi
  • Viongozi 7 wa upinzani washikiliwa na polisi kwa tuhuma za ugaidi ikiwemo kuchoma moto vituo vya mafuta, ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) pamoja na ofisi zingine za serekali

Viongozi saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanashikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam wakishukiwa kupanga njama za kuchoma vituo vya mafuta, masoko, ofisi za serikali, kuhujumu miundombinu ya barabara kwa kuchoma matairi na ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, asema polisi inawashikilia viongozi saba wa upinzani kwa tuhuma za ugaidi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amedhibitisha taarifa hizo leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti, Mambosasa amesema viongozi hao wanashikiliwa kwa makosa ya ugaidi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Amewataja wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam Issaya Mwita, aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacoba, aliyekuwa Mbunge wa Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema.

Wengine ni mwanachama Abwines Kichengwa, Elisha Mangauka na  Godfrey Mkandala ambaye pia ni msaidizi wa aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Taarifa hizi zinaendelea kutoka, usipitiwe bofya hapa: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa