Viongozi tisa wa upinzani wakubali ushindi wa Dk. Magufuli

01Nov 2020
DODOMA
Nipashe Jumapili
Viongozi tisa wa upinzani wakubali ushindi wa Dk. Magufuli
  • "... kwa niaba ya viongozi wengine wa upinzani, sisi sote tuko tayari kushirikiana na Rais Dk. John Magufuli" Queen Cuthbert Sendiga (ADC)

Angalau viongozi 9 wa kambi ya upinzani ambao pia walikuwa wakigombea ofisi ya mtendaji wametoa taarifa ya pamoja kukubali Dk John Magufuli kama mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Angalau viongozi 9 wa kambi ya upinzani ambao pia walikuwa wakigombea ofisi ya mtendaji wametoa taarifa ya pamoja kukubali Dk John Magufuli kama mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Akihutubia mkutano huko Dodoma ambapo rais mteule anatarajiwa kupokea cheti chake cha ushindi wa urais, Queen Cuthbert Sendiga, mgombea urais kutoka Alliance for Democratic Change (ADC) alisema viongozi hao wapo tayari kutoa ushirikiano.

"... kwa niaba ya viongozi wengine wa upinzani, sisi sote tuko tayari kushirikiana na Rais Dk. John Magufuli," alisema Queen Cuthbert Sendiga.

Katika sherehe hizo pia alikuwepo rais wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya ambaye aliongoza kundi la waangalizi wa kimataifa ambao walisimamia mchakato wa uchaguzi.

"Bila amani, bila haki hakuwezi kuwa na ushindi," alisema. "Uchaguzi ulipangwa vizuri sana, na tunwapongeza watu wa Tanzania kwa kufanya uchaguzi wa amani na haki," alihitimisha.

Endelea kufuatilia #Uchaguzi 2020 https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa