Viongozi wa dini waonywa kutumia nyumba za ibada kufanyaa siasa

27Sep 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es salaam
Nipashe Jumapili
Viongozi wa dini waonywa kutumia nyumba za ibada kufanyaa siasa

Viongozi wa Dini wa Kamati ya Amani wamelaani vikali vitendo vya baadhi ya Viongozi wa Dini kutumia Madhabahu na Nyumba za ibada kufanya kampeni za kuwanadi viongozi wa siasa jambo ambalo ni kinyume na maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 26,2020, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum amesema kama vitendo hivyo vitafumbiwa macho vinaweza kuhatarisha hali ya amani na kuwagawanya waumini wanaokwenda kusali.Aidha amesema kama kiongozi wa dini anaona mgombea fulani anamfaa ni vyema akaenda kwenye majukwaa ya siasa ili kumnadi lakini sio kutumia nyumba za ibada kunadi wanasiasa.

 

Habari Kubwa