Viongozi watakaosababisha kuwepo kwa migogoro ya ardhi hawatavumiliwa

26Sep 2021
Julieth Mkireri
Pwani
Nipashe Jumapili
Viongozi watakaosababisha kuwepo kwa migogoro ya ardhi hawatavumiliwa

​​​​​​​MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, amesema hawatawavumilia wajumbe wa Baraza la Ardhi ambao hawatafuata sheria na kusababisha kuendelea kuwepo kwa migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.

Kunenge ameyasema hayo Jana alipokua akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM Julai 2020 hadi June 2021) katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika Kibaha.

Amesema wajumbe wa Baraza hilo walioapishwa kwa kila Wilaya watapimwa na atayavunja muda wowote endapo hayatafuata sheria.

"Baadhi ya watendaji na wananchi hatuheshimu na kufuata sheria, tusimamie sheria kumaliza migogoro ya ardhi" amesisitiza RC Kunenge.

Aidha, amesema akifika sehemu ambayo wananchi wanalalamikia uwepo wa migogoro ya ardhi hatamuacha mtendaji ambaye hajatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Habari Kubwa