Vitabu 22,553 vya masomo ya sayansi vyamwangwa shule za msingi 72

26Mar 2020
Shaban Njia
KAHAMA
Nipashe
Vitabu 22,553 vya masomo ya sayansi vyamwangwa shule za msingi 72

HALMASHAURI ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, imepokea na kugawa vitabu vya masomo mbalimbali zaidi ya 22,553 vikiwemo vya masomo ya sayansi vya mtaala mpya katika shule za msingi 72 ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hizo.

BAADHI ya walimu wa kuu wa shule za msingi, Halmashauri ya mji wa kahama,wakichukua vitabu vya mtaala mpya kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la sita, awali na darasa la pili vya masomo mbalimbali vikiwemo vitabu vya Sayansi na kiongozi kwa walimu, PICHA: NA SHABAN NJIA

Vitabu hivyo vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi huku zaidi ya vitabu 20,188 vikiwa vya darasa sita na miongozo kwa walimu,ambapo hapo awali walimu walikuwa wakiandaa masomo kwa kutumia vitabu vilivyopo kwenye mitandao.

Akigawa vitabu hivyo Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Shule za Msingi kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Sadick Juma alisema kuwa, kila mwanafunzi atapatiwa kitabu na atakae poteza mzazi au mlezi atawajibika kukilipa au kukirejesha kabla ya muhura haujamalizika.

Aidha alisema kuwa,wamegawa vitabu vya mtaala mpya vya masomo ya Kiswahili, Hesabu, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii,Uraia na Maadili na vitambu vya lugha ya kiingereza na kila somo vikiwa vitabu 2,884 kwa darasa la sita pekee sawa na vitabu 20,188.

Pia alisema kwa, darasa la awali wamegawa vitambu 242 kwa kila somo la Hisabati, Kuandika,Kusoma na Michezo na sanaa huku darasa la pili wakigawa vitabu 223 vya masomo ya Afya na Mazingira, Hisabati, Kuandika, kusoma pamoja na michezo na sanaa.

“Kama mwanafunzi anaweza kutunza daftari la darasa la kwanza mpaka anafika darasa la saba bado anakuwa nalo,basi akipatiwa kitabu hiki ataweza kukitunza,kwa mwanafunzi atakaepoteza kitambu hiki mzazi wake au mlezi atawajibika kukiripa”Alisema Juma.

Anaongeza kuwa”Lengo la kugawa vitabu hivi kwenye shule zetu za msingi zote 72 ni kuhakikisha vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vitabu vya miongozo kwa walimu zinapatikana na kuwapunguzia gharama walimu kuandaa masomo kwa njia ya mitandao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu Wakuu, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Malunga, Beatrice Katama alisema kuwa,vitabu hivyo vitasaidia kuondoa changamoto ya ukosefu wa vitabu vya masomo ya sayansi vya mtaala mpya hasa kwa darasa la sita,awali na darasa la pili.

Hata hivyo alisema kuwa,hapo awali walikuwa wakiandaa masomo kwa njia ya vitabu vya mitandaoni na kutumia gharama kubwa wakati wa maandalizi ikiwemo wanafunzi zadia ya watau kuchangia kitabu kimoja wakati wa masomo na kusababisha baadhi ya wafunzi kukosa vitabu.

Habari Kubwa