Waajiri watakiwa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa, ajali kazini

21Nov 2020
Na Mwandishi Wetu
ARUSHA
Nipashe
Waajiri watakiwa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa, ajali kazini
  • Watakiwa kutoa ushirikiano kwa OSHA ili kuhakikisha suala hilo linatekelezwa bila vikwazo....

KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amewasisitiza waajiri mkoani humo kuweka mifumo madhubuti ili kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali katika maeneo yao ya kazi.

Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega (Katikati) ambaye ni Mgeni rasmi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Vision Zero, akiwa na Mkurugezi wa Usalama na Afya Mhandisi Alex Ngata Pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti na Takwimu OSHA, Joshua Matiko.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo Novemba 21,2020 Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Vision Zero yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) jijini Arusha, amesema uwepo wa mifumo mizuri maeneo ya kazi itasidia kuwakinga wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali zinazotokea maeneo ya kazi.

Amesema wafanyakazi ni kipuri namba moja kwa tassisi au kampuni yeyote katika ufanisi wa kazi yeyote, na kusisitiza kuwa wafanyakazi wana mchango mkubwa sehemu ya kazi hivyo hawana budi kuhakikisha wanawalindwa dhidi ya magojwa na ajali zinazoweza kutokea sehemu za kazi ili kuwawezesha kufikia malengo waliojiwekea.

Mhandisi Alex Ngata akiongea kwenye mafunzo ya Vision zero yaliofanyika mkoani Arusha.

Katibu Tawala huyo amewataka waajiri kutoa ushirikiano kwa OSHA ili kuhakikisha suala hilo linatekelezwa bila vikwazo, kwani wafanyakazi ndio watendaji wa kazi, endapo ushirikiano utakuwepo baina yao, itasaidia kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi.

“Suala hili ni la pande tatu yaani mwajiri,mwajiriwa, na serikali na endapo ushirikiano huo utadumishwa basi ajali na magonjwa yatapungua ama kuisha kabisa sehemu za kazi”  amesema

Baadhi ya Wawakilishi wa Viwanda, wafanyabiashara, taasisi na kampuni za  Mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini, mafunzo ya Vision zero yaliyotolewa na OSHA mkoani Arusha.
Baadhi ya Wawakilishi wa Viwanda, wafanyabiashara, taasisi na kampuni za  Mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini, mafunzo ya Vision zero yaliyotolewa na OSHA mkoani Arusha.

Hata hivyo amewataka wafanyakazi kujenga utamaduni wa kujilinda wenyewe wakiwa kazini, kwani wao wanabeba jukumu kubwa la kujilinda dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi kutokana na majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Usalama na Afya OSHA, Mhandisi Alex Ngata amesema, Kampeni ya Vision Zero ni kampeni ya kidunia, nchi mbalimbali dunia nizinatekeleza kampeni hii, na lengo kuu la Vision zero ni kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi.

Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Vision Zero mkoani Arusha.

Mhandisi Ngata amesema uwepo wa mfumo sehemu za kazi  utawawezesha waajiri kujikagua wenyewe, na hivyo kuweza kuzuia magonjwa na ajali sehemu za kazi.

“Mfanyakazi ni msingi imara katika biashara na uzalishaji ambao OSHA unaungalia bila wao hawawezi kuzalisha na kufanyabiashara hivyo ni muhimu kuzingatia usalama na afya zao wakiwa kazini na kuwepo mfumo wa kulinda nguvu kazi hiyo”. amesema Mhandisi Ngata

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema, Vision zero itawasaidia kuweka mifumo mizuri ya kuwalinda wafanyakazi juu ya ajali na magonjwa sehemu za kazi.

 “Kama mwajiri atatekeleza kama ambavyo vision zero inataka, kuondoa magonjwa na ajali sehemu za kazi, na kama utafuata maelekezo, natumaini tutazalisha sana sehemu za kazi na hivyo kuongeza pato la taifa, na ukisema umeondoa ajali na magonjwa sehemu za kazi , hata wafanyakazi watakuwa na moyo wakufanya kazi zaidi na pia watakuwa nguvu za kufanyakazi zaidi, tutawashawishi waajiri wetu watekeleze kama ambavyo lengo kubwa la Vision zero linataka,.” amesema Emmanuel Mvamila mwakilishi wa kiwanda cha TPC Moshi.

Vision zero ni Kampeni ya Kidunia iiliyoanzishwa kwa lengo ya kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi,kampeni hiyo inazitaka maeneo ya kazi kuweka mifumo ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi, na kampeni hii inatekelezwa kwenye mataifa mbalimbali duniani.

 

Habari Kubwa