Wabunge watoro wa vikao wakalia kutikavu

21Feb 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Wabunge watoro wa vikao wakalia kutikavu

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa, ameagiza wabunge wote  wa chama hicho mkoani humo, ambao hawaja hudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa waandike barua za maelezo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye kikao cha halmashauri kuu ya CCM Mkoa.

Magesa amebainisha hayo Leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa, kilichokuwa na lengo la usomaji wa taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, kuanzia kipindi cha Januari 2016- Disemba 2019.

Amesema haiwezekani baadhi ya wabunge wa mkoa huo wasiwepo kwenye kikao hicho, bila ya kutoa taarifa yoyote na wakati wao ni wajumbe muhimu wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.

"Naagiza Makatibu wa Wilaya wa Chama cha Mapinduzi CCM, mkalisimamie hili wabunge wote ambao hawaja hudhulia kwenye kikao hiki cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa, waandike barua za maelezo," amesema Magesa.

"Na bahati nzuri mimi ndio msimamizi wa uchaguzi ngazi ya chama, na wasipo hudhulia kikao kingine nitajua nini cha kufanya, wasifanye chama kuwa lifti ya mafanikio yao," ameongeza.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Malolwa akizungumza kwenye kikao hicho cha halmashauri ya CCM Mkoa, ya usomaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM.

Aidha wabunge walio hudhulia kikao hicho ni Elias Kwandikwa Jimbo la Ushetu, Ezikiel Maige, Msalala na Azza Hilali Mbunge wa Vitimaalum.

Wabunge ambao hawakuhudhulia ni Stephen Masele, Shinyanga mjini, Ahmed Salum, Solwa, Jumanne Kishimba Kahama mjini, Seleman Nchambi Jimbo la Kishapu, na Ruth Mayenga Mbunge Vitimaalum.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi amesema imetekelezwa kwa kiwango kikubwa ikiwamo sekta ya kilimo, elimu, afya,maji, viwanda, ardhi, madini, Nishati na barabara.

 

 

 

 

 

 

 

 

Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige, akichangia hoja kwenye mkutano huo na kupongeza namna utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ilivyotekelezwa kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM, kuanzia 2016 hadi Desemba 2019.

 

Habari Kubwa