Waajiri wadaiwa sugu mifuko ya jamii kutangazwa hadharani

29Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Waajiri wadaiwa sugu mifuko ya jamii kutangazwa hadharani

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, amewaagiza Mameneja wa mikoa wa NSSF na PSSF kuhakikisha kuwa hakuna madeni kwa waajiri na ambao wana madeni wachukuliwe hatua.

Katambi amesema hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa waajiri ambao wamekuwa wakileta ujanjaujanja na unapofika muda wa kustaafu mfanyakazi anasumbuliwa pesa zake za mafao.

“Hili la wadaiwa sugu au waajiri sugu wasiolipa mishahara, kodi (P.A.Y.E) na michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii tutawatangaza kumi bora hadharani na kuwapa tuzo ya hati chafu ya kutotii sheria za kazi”

“Natoka shukrani za dhati kwa niaba ya Waziri Mkuu wetu Kasimu Majaliwa na Waziri wa Nchi Jenista Mhagama kwa TUCTA na ATE kwa ushirikiano wao mkubwa na kusimamia haki za Wafanyakazi wa Tanzania” amesema Katambi.

Habari Kubwa