Wadakwa tuhuma wizi wa simu mchezo Simba na Mwadui

19Apr 2021
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Wadakwa tuhuma wizi wa simu mchezo Simba na Mwadui

JESHI la Polisi Mkoani Shinyanga, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za wizi wa simu kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Simba na Mwadui, uliochezwa katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani humo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba, akitoa taarifa leo kwa vyombo vya habari, na kusema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 10 jioni, wakati timu hizo mbili zikiendelea kucheza mpira.

Amesema watu hao walikatwa na askari, ambao walikuwa doria wakihakikisha ulinzi na usalama katika mchezo huo wa ligi kuu, ambapo walikuwa wameiba simu aina ya iPhone 5 S7,Infinix Hot 8, Sony Expirial, Itel ndogo, pamoja na Tecno.

"Watu tulio wakamata ni Amosi Shija, Gerald Abdallah, na Rashid Hamisi, ambapo wote tutawafikisha Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika," amesema Magiligimba.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa wananchi ambao waliibiwa simu zao, wafike katika kituo kikubwa cha Jeshi la Polisi mkoani humo ili kuzibaini.

Habari Kubwa