Wadau wa Afya Shinyanga wachangia vifaa kinga vya Corona

07Apr 2020
Dotto Lameck
Shinyanga
Nipashe
Wadau wa Afya Shinyanga wachangia vifaa kinga vya Corona

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kwa kushirikiana na wadau wa afya pamoja na Shirika la Touch Foundation wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 10.7 kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile kwa ajili ya kuzigawa katika halmashauri za Wilaya ili kujikinga-

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, Sriex Premium Latex.

-kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa kutoa matibabu.

Makabiziano hayo ya yamefanyika jana April 6, 2020 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, huku akiwashukuru wadau wote wa afya waliochangia kupatikana kwa vifaa hivyo wakiongozwa na Shirika la Touch Foundation iliyotoa shilingi milioni 10.4 na wadau wengine walichangia shilingi 300,000/= na kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona kwa wauguzi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Methylated Sprit ‘Sanitizer’

“Tunawashukuru wadau wanaotambua mchango wa afya katika Mkoa wetu, nakumbuka siku ya Ijumaa wiki iliyopita tulikaa kikao cha pamoja nao na waliahidi,na mmoja kati ya wadau walioahidi moja kwa moja ni Touch Foundation tunawashukuru ahadi yao leo imetekelezeka kwa kuchangia shilingi milioni 10.4”

“Tumeshatoa elimu ya kutosha na hakuna mahali ambapo hatujapita sasa ni wakati wa kuchukua hatua na wale ambao kwa makusudi wanakataa kunawa tuchukue hatua, tupige faini na wale wanaokaidi kabisa tupeleke kituo cha polisi ili hatua nyingine zichukuliwe ili tuiache Shinyanga ikiwa salama na nchi kwa ujumla kutokana na Corona”,amesema Telack

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kunawa na kuzingatia ushauri unaotolewa na Wizara ya Afya.