Wadau wa semina za jinsia watoa mapendekezo ya bajeti ya Taifa

23Jun 2022
Yasmine Protace
The Guardian
Wadau wa semina za jinsia watoa mapendekezo ya bajeti ya Taifa

WADAU wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wametoa mapendekezo yao kwa serikali juu ya nini kifanyike baada ya kutathimini bajeti ya afya mwaka 2022/23 kwa mlengo wa kijinsia.

Mapendekezo yao yanakuja baada ya TGNP Mtandao kutoa tamko lao kupitia vyombo mbalimbali vya habari juu ya bajeti ya Taifa kwa mtazamo wa kijinsia.

Katika semina za GDSS ambazo uratibiwa na TGNP Mtandao,waliangalia Mambo mbalimbali yaliyotajwa katika bajeti ya Taifa ikiwamo kuondoa ada kwa kidato cha tano na sita.

Mambo mengine walioangalia katika bajeti hiyo ni pamoja na kujengwa kwa vyuo vya veta katika mikoa isiyo na vyuo, serikali kutoa mikopo ya magari kwa watumishi wake, serikali kufanya mikutano kwa njia ya mitandao ili kupunguza matumizi.

Pia, waliangalia katika bajeti hiyo,Ofisi ya CAG kuongezwa fedha,serikali kujenga daraja la juu jangwani,anayeshushwa cheo kupunguzwa mshahara, mikopo kutolewa kwa wamachinga na kutengwa kwa pesa kwa ajili ya sensa.

Habari Kubwa