Waendesha baiskeli 35 wawasili Tanga wakitokea Dar

06Jul 2020
Boniface Gideon
Tanga
Nipashe
Waendesha baiskeli 35 wawasili Tanga wakitokea Dar

Zaidi ya waendesha baiskeli 35 kutoka jijini Dar es Salaam, wamewasili mkoani Tanga baada ya kuendesha kwa siku tatu.

Lengo la kutembea kwa baiskeli kutoka Dar es Salaam, hadi Tanga nikutangaza utalii na kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vya utalii.

Kiongozi wa msafara huo, Abdul Mohammed, amesema wanatarajia kutembea zaidi ya kilomita 1,400 na wanatarajia kumaliza safari mwezi oktoba mkoani Mara.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa, amewapongeza kwa kujitoa kutangaza utalii wa ndani na amewatakia heri katika safari yao yakuelekea mkoani Mara.

Katika safari hiyo wamo watoto chini ya miaka kumi.

Habari Kubwa