Wafamasia Simiyu watakiwa kujitathimini

12Aug 2020
Happy Severine
SIMIYU
Nipashe
Wafamasia Simiyu watakiwa kujitathimini

Wafamasi mkoani Simiyu wametakiwa kujitathimi katika utendaji wao, ili kuhakikisha kuwa wanadhibiti matumizi ya dawa na vifaa tiba yasiyo sahihi katika vituo vyao vya kazi.

mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwa katika kikao kazi cha wafanyakazi wa idara ya afya wa tatu kushoto ni katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Mariam Mmbaga.

Hayo yamesemwa jana leo na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika kikao kazi na wafanyakazi wa idara ya afya kilichofanyika mjini Bariadi.

Mtaka amesema, wafamasia wanabidi wajitume katika kutimiza majukumu yao na  kutambua katika sekta ya  dawa kuna changamoto kadha wa kadha.

Ameongeza kuwa ni wazi kuwa anataarifa kwa baadhi ya  wafamasia ambao hawafanyi kazi zao vizuri hivyo wanaipa hasara serikali jambo ambalo sio lengo la serikali kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya  Ukaguzi wa Mnyororo wa ugavi Dk. Festo Dugange, amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi ni kudhibiti matumizi mabaya ya dawa ili kuboresha vifaa katika vituo vya afya pamoja na kubaini hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

" Tumebaini uzembe uliopelekea ugumu wa kutambua uhalali wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa uliosababishwa na ubovu wa utunzaji wa kumbukumbu," amesema.

Habari Kubwa