Wafanyabiashara Mtwara watishia kugeuza soko jengo la ibada

08May 2021
Abdallah Khamis
MTWARA
Nipashe
Wafanyabiashara Mtwara watishia kugeuza soko jengo la ibada

WAFANYABIASHARA Katika soko jipya la Chuno katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara, wametishia kuligeuza jengo la soko hilo kuwa nyumba ya ibada kwa madai ya kushindwa kufanya biashara kutokana na kukosa wateja.

SOKO LA CHUNO MKOANI MTWARA.

Wakizungumza  mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Kanali Emanuel Mwaigobeko, wafanyabiashara hao wakiongozwa na Issa Hassan, wameeleza kuwa eneo hilo limekuwa gumu kwao kufanya biashara kutokana na baadhi yao kushindwa kuhamia katika soko hilo na kubaki katika soko la Sabasaba mkoani humo.

Hassan ametaja kero zingine katika soko hilo la Chuno kuwa ni pamoja na magari yanayopaswa kushusha mizigo sokoni hapo kukataa kufika katika soko hilo na badala yake kushusha mizigo katika soko la zamani.

"Mkurugenzi,sisi si kama hatutaki kufuta sheria, lakini ninyi mlipozindua soko hili lengo lilikuwa ni kuwafanya wafanyabiashara wote kuwa sehemu moja lakini leo wengine wamebaki soko la zamani na hata magari yanayopaswa kushusha mizigo huku, hayataki kuja yanaenda sabasaba” amesema Hassan na kuongeza kuwa;

“Kwa mwenendo huu tunaoenda nao kama hamtatafuta suluhu ya haraka, sisi tutaligeuza hili soko kuwa jengo la ibada na tutaanza kufanya ibada siku ya Iddi, kwa kuwa mpaka wakati huo tunaamini hakutakuwa na mfanyabiashara aliyeweza kulinda mtaji wake kutokana na mwenendo usioridhisha wa biashara”amesema 

Habari Kubwa