Wafanyabiashara Tanzania ruksa kuwekeza Kenya

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe Jumapili
Wafanyabiashara Tanzania ruksa kuwekeza Kenya

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, amewasihi wafanyabiashara wa Tanzania kuendelea kufanya biashara na kwenda kuwekeza nchini Kenya kwa kufuata sharia, taratibu na miongozo iliyowekwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku akiwataka kuwasiliana na Wizara endapo-

-kama watakutana na changamoto ya aina yoyote.

Hayo ameyasema katika Mkutano wa tano (5) uliofanyika baina ya Tanzania na Kenya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru (NTBs) baina ya nchi hizo uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Katika mkutano huo Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Mkumbo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano huo ambao ulijumuisha Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, wakati ujumbe wa kenya ukiongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali, Betty Maina, aliyeambana na Balozi wa Kenya nchini Tanania.

Prof. Mkumbo amesema kuwa mkutano huo ni utekelezaji wa maelekezo ya kuimarisha mahusiano ya biashara na nchi jirani yaliyotolewa katika Ziara ya Kiserikali iliyofanywa nchini Kenya na, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tarehe 4-5 Me8i, Mwaka huu.

Prof. Mkumbo amesema Mkutano huo wa kibiashara baina ya nchi hizo ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya biashara katika sekta za kilimo, forodha, uhamiaji na usafirishaji. Jumla ya masuala 64 yamejadiliwa ambapo kati ya hayo masuala 30 yametatuliwa na mengine 34 yaliyobaki yamewekewa mkakati maalum na muda wa utekelezaji.

“Miongoni mwa masuala yaliyotatuliwa kwa upande wa Tanzania ni pamoja na kuwezesha upitishaji wa bidhaa mpakani, hususan vinywaji baridi kama vile juisi kutoka Tanzania kwenda Kenya, kuondolewa kwa tozo za ukaguzi (inspection fees) zilizokuwa zinatozwa na Mamlaka za Kenya kwenye bidhaa za Tanzania, ikiwemo unga wa ngano, zenye alama ya ubora kutoka Mamlaka husika Tanzania, kuwezesha upitishaji wa mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya na Kuondoa ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za kioo kutoka Tanzania kwenda Kenya.” amefafanua Prof. Mkumbo.

Habari Kubwa