Wafanyabiashara wanaoficha mafuta waonywa

14Jan 2021
Mohab Dominick
Kahama
Nipashe
Wafanyabiashara wanaoficha mafuta waonywa

SERIKALI wilayani Kahama, mkoani Shinyanga imewaonya wafanyabiashara wa mafuta ya kula wanaoficha bidhaa hiyo na kuwataka wayatoe katika maghala yao na kuyauza kwa wananchi.

Kukosekana kwa bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali kumesababisha kupanda kwa bei na kukosekana katika maduka yaliopo katika maeneo hususani katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, alitoa onyo hilo juzi wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi.

Macha alisema bei ya mafuta katika Wilaya ya Kahama imepanda kwa kiasi kikubwa na kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wametumia mwanya huo kuficha bidhaa hiyo na kuleta ugumu kwa walaji wa mji huo.

Alisema baadhi ya viwanda vya mafuta katika maeneo mbalimbali vimekosa uzalishaji kutokana na kukosa malighafi ambayo ni mbegu, huku akisisitiza wakulima kulima mazao ambayo yatakuwa yakitoa bidhaa hiyo kupitia mbegu zake kama alizeti na pamba.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa