Wafanyakazi Mwanza walalamika ushuru wanayokatwa kwenye mapato ghafi

15Sep 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Wafanyakazi Mwanza walalamika ushuru wanayokatwa kwenye mapato ghafi

WAFANYABIASHARA mkoani Mwanza, wamelalamikia tozo ya ushuru wa huduma (Service Leavy) wanayokatwa kwenye mapato ghafi inawaumiza na inachangia kuua mitaji yao na biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.

Malalamiko hayo waliyaibua  katika leo na Baraza la Biashara la mkoa walisema tozo ya ushuru wa huduma ya asilimia 0.3 inayotolewa kwenye mapato ghafi kunaua mitaji yao na kuishauri serikali ushuru huo ukatwe kwenye faida.

Wamesema tozo hiyo si rafiki, hivyo ipo haja serikali ikapeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ili tozo hiyo ikatwe kwenye faida badala ya mapato ghafi ili kulinda mitaji yao, vinginevyo uwezo wao wa kuchangia uchumi na mapato ya serikali utapungua.

Mkurugenzi wa JAEGS Ltd, Dk. Elibariki Mmari,amesema kutoza ushuru wa huduma chini ya asilimia 0.3 hakukiuki sheria na kutolea mfano mikoa ya Iringa na Mbeya inatoza asilimia 0.1.

“Suala la tozo ya ushuru wa huduma tumelilalamikia kwenye baraza tangu mwaka 2013 hadi leo,tatizo ni uelewa wa kutafsiri sheria, sheria inaelekeza isiyozidi asilimia 0.3 hata halmashauri zingine zinatoza asilimia 0.2 na nyingine 0.2,hakuna haja ya kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni,” alishauri Dk.Mmari.

Alisema baraza liziambie halmashauri zikae na wafanyabiashara ili kuangalia namna ya kupunguza ushuru huo wa huduma bila kwenda bungeni kubadilisha sheria.

Naye Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vituo vya Afya Binafsi, Dk. Felician Ndauzi, amesema changamoto zao nyingi zinahitaji ufumbuzi huku zingine zikihitaji marekebisho ya sheria lakini pia kuwe na mawasiliano na serikali ili biashara ifanyike vizuri kwa kuwa biashara ssa inafanyika kimtandao.

Meneja wa Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo amesema biashara kufanyika kimtandao ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara katika kukuza uchumi na kwa kuwa TRA wanatumia teknolojia ya  mawasiliano watalifanyia kazi.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wenye Viwanda (TCCIA) Mkoa wa Mwanza, Mwita Kinene, amesema serikali kuwacheleweshea wazabuni malipo ya huduma kunasababisha walipe riba kubwa kwenye taasisi za fedha.

Pia amesema kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa vifaa vya Mashine za Kielekroniki (EFD’s)kwani mtoa huduma huyo ni mmoja na hivyo kusababisha kero na usumbufu kwa wafanyabiashara na kudai baadhi ya watumishi wa TRA wanaitumia mamlaka hiyo vibaya.

“Kuja kenye vikao si kutuhumiana bali wakupata uelewa wa pamoja,kuna wafanyabiashara wa wadogo,kati na wakubwa,makundi hayo yote yana kero na changamoto nyingi ukizingatia zinakinzana na sheria,”alissema Kinene na kushauri ziorodheshwe kwenye mabaraza ya wilaya na kuletwa kwenye baraza la mkoa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema changamoto za wafanyabishara hao watazifanyia kazi ma kuwataka watumishi wa umma kupunguza urasimu na kushawishi rushwa kwa wawekezaji ili wapewe maeneo ya kuwekeza.

Amesema vitendo hivyo vinachangia wawekezaji kushindwa kuwekeza sababu ya urasimu na rushwa ama njo kesho kunakofanywa na watumishi wa umma wenye dhamana hiyo,ili kufanikiwa kwenye uchumi wa bluu halmashauri zitenge maeneo hayo mapema.

Pia wafanyabiashara hao wamelalamikia kitendo cha wafanyabiashra wadogo (machinga) kupanga bidhaa na kufanya biashara mbele ya maduka yao, kunawadhoofisha na wanapunguza mapato ya serikali kwa kuwa wanalipa kodi na ushuru mbalimbali.

Habari Kubwa