Wafungwa 385 Dodoma waachiwa huru

10Dec 2019
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Wafungwa 385 Dodoma waachiwa huru

JUMLA ya wafungwa 385 wa magereza mbalimbali ya mkoa wa Dodoma, wameachiwa huru kutokana na msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa jana katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru.

Akihakiki orodha ya wafungwa waliostahili kupata msamaha huo leo katika Gereza la Isanga,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bilinith Mahenge amewataka wafungwa hao kwenda kuwa raia wema wanaozingatia kanuni, taratibu na katiba ya nchi.

Amesema Rais Magufuli ametoa msamaha huo kwao hivyo hawana bodi kwenda kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji kama walivyofundishwa wakati wakiwa gerezani.

Kwa upande wake mkuu wa magereza mkoa ACP Keneth Mwambije, amesema wafungwa hao wanatoka katika gereza la Isanga, Kongwa,Msalato,Kondoa,Mpwapwa na King'ang'a.

Amesema wafungwa wamekuwa wakipewa mafunzo mbalimbali ya ujenzi, kilimo,na kazi za mkono kama ufumaji wa vitambaa na vikapu.

Akitoa neno la shukrani mmoja wa wafungwa Abdalah Ramadhan aliyefungwa miaka 30 kwa kosa la ubakaji amemshukuru Rais Magufuli na kusema wamejirekebisha na kuahidi kwenda kuwa raia wema.

Habari Kubwa