Wafyeka pori kujenga zahanati Geita

27May 2020
Dotto Lameck
Geita
Nipashe
Wafyeka pori kujenga zahanati Geita

WAKAZI wa Kata ya Bombambili mkoani Geita, wamejitolea kufyeka pori kwa ajili ya kujenga zahanati katika eneo hilo kwa lengo la kuondoa adha zinazowakabili akinamama wajawazito kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, amesema wameweka mpango maalumu wa kuunga mkono wananchi hao walioamua kujenga zahanati katika kila kijiji ili kuhakikisha majengo yote yanakamilika kwa wakati ili kuwaepusha wananchi kuepuka na adha ya huduma ya afya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinari, ameahidi kutoa tofali zaidi ya Elfu 20 pamoja na saruji ili kuwezesha kukamilika kwa zahanati hiyo.

Habari Kubwa