Wagombea udiwani 24 warejeshwa

14Sep 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Wagombea udiwani 24 warejeshwa

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imepitia, kuchambua na kufanyia kazi rufani 46 za wagombea udiwani ambao hawakuridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa dhidi yao na kukubali kuwarejesha 24.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera, rufani 22 zimekataliwa.

Alizitaja kata zilizokubaliwa rufani na majimbo kwenye mabano kuwa ni Dunda (Bagamoyo), Mtwivila (Iringa Mjini), Kikilo (Kondoa), Makurumla (Ubungo), Hezya (Vwawa), Makorongoni (Iringa Mjini) na Bwawani (Arumeru Magharibi).

Nyingine ni Jinjimili (Magu), Kimnyaki (Arumeru Magharibi), Lemanyata (Arumeru Magharibi), Mkwawa (Iringa Mjini), Kisarawe II (Kigamboni), Makurumla (Ubungo), Mbabala (Dodoma Mjini), Mpanda Hoteli (Mpanda Mjini).

Lusungo (Kyela), Same (Same), Maisaka (Babati Mjini), Makuburi (Ubungo), Kibada (Kigamboni), Maore (Same Mjini) na rufani tatu kutoka kaya ya Mshindo (Iringa Mjini).

Pia NEC imekataa rufani 13 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa, kata na majimbo kwenye mabano kuwa ni Kawanjense (Mpanda), Mjini Chorombola (Ulanga), Mabokweni (Tanga Mjini), Chanika (Karagwe), Mwamala (Manonga) na Kiomboi (Iramba Magharibi).

Nyingine ni Mwasenkwa (Mbeya Mjini), Old Iranga (Iramba Magharibi), Magara (Babati Vijijini), Arri (Babati Vijijini), Chapwa (Tunfuru) na mbili kutoka Kaya ya Kibamba (Kibamba).

Vile vile, taarifa hiyo ilisema kuwa rufani tisa za kupinga walioteuliwa ni Nonde (Mbeya Mjini), Mwagata (Iringa Mjini), Mabibo (Ubungo), Mkimbizi (Iringa Mjini), Kipanga (Sikonge), Nsoho (Mbeya Mjini), Ilmela (Mbeya Mjini), Bagara (Babati Vijijini) na Nkinga (Manonga).

Pia Tume hiyo imefanyia kazi rufani 113 za wagombea ubunge.

Rufani 149 za udiwani zimefanyiwa kazi ikiwamo zilizotolewa maamuzi mwishoni mwa wiki kwa madiwani 24.

Habari Kubwa