Wagonjwa wa dengue wapungua

04Jul 2019
Romana Mallya
Dar es Salaam
Nipashe
Wagonjwa wa dengue wapungua

WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, jana aliwaongoza wakazi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam-

kupulizia dawa ya kuua mazalia ya mbu waenezao ugonjwa wa dengue na kueleza kuwa idadi ya waliougua imepungua kutoka watu 2,759 mwezi Mei hadi wagonjwa 790 mwezi uliopita.

Waziri Ummy alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Mkurugenzi na Mbunge wa jimbo hilo, kwa hatua walizochukua za kukabiliana na ugonjwa huo.

"Nimeridhishwa na hatua mlizochukua za kununua mashine mpya 14 za kupulizia dawa, wamenunua viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 kwa Sh. milioni 53, wamenunua lita 210 za kuua mbu wapevu na upuliziaji unaendelea katika Kata 25," alisema.

Waziri Ummy alisema matokeo ya jitihada walizofanya zimeanza kuonekana kwa sababu idadi ya wagonjwa wilayani humo imepungua kutoka 527 mwezi Mei hadi 207 mwezi uliopita.

"Ninawataka na kuwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika kutokomeza mbu," alisema.

Habari Kubwa