Wagundulika na TB, VVU

10Dec 2016
Gideon Mwakanosya
Songea
Nipashe
Wagundulika na TB, VVU

WATU 129 wamegundulika kuwa na kifua kikuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.

waziri wa afya ummy mwalimu.

Ofisa Habari wa Manispaa hiyo, Albano Midelo, alisema jana kuwa watu hao wamebainika baada ya Idara ya Afya kuendesha uchunguzi wa maambukizi ya ugonjwa huo kati ya Aprili hadi Juni , mwaka huu.

Midelo alisema watu hao walibainika katika upimaji uliofanyika katika vituo vitano kwa kutumia njia ya sampuli za makohozi na kwa njia ya kupiga mionzi mikali (X-Ray).

Alisema katika watu hao waliopimwaa, 51 kati yao sawa na asilimia 51.9 waligundulika kuwa na virusi vya Ukimwi (VVU).

Hata hivyo amesema wagonjwa walioambukizwa kifuu kikuu mwaka huu wamepungua kulinganisha na watu 143 waliogundulika katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni, mwaka jana.

Manispaa ya Songea ina vituo 22 vinavyopokea wagonjwa baada ya ugunduzi wa magonjwa ya kifua kikuu ambavyo vimepewa huduma shirikishi karibu na makazi ya wagonjwa husika.

Habari Kubwa